Na ENGLIBERT KAYOMBO – WAF, Dar Es Salaam.

Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametoa rai kwa wananchi kuchanja chanjo dhidi ya UVIKO-19 ili Tanzania iwe na watu wengi waliochanja na kupata Kinga ya Jamii dhidi ya UVIKO-19.

Waziri Ummy Mwalimu amesema hayo leo Jijini Dar Es Salaam mara baada ya kutembelea Maonyesho ya Kimataifa ya 46 ya Biashara ya Saba Saba akiwa pamoja na Mratibu wa Kimataifa wa Mapambano dhidi ya UVIKO-19 kutoka umoja wa Mataifa Dkt Ted Chaiban ambapo walitoa elimu na hamasa ya chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa wananchi.

“Chanjo dhidi ya UVIKO-19 ni salama na haina madhara na ili tuweze kupata kinga dhidi ya Ugonjwa huu wa UVIKO-19 ni lazima tuchanje” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy amesema kwamba ili Duniani tuweze kuwa na Kinga ya Jamii na kuudhibiti ugonjwa wa UVIKO-19 inatubidi angalau asilimia 70 ya watu