Na Mwandishi wetu - Arusha

Tanzania Kama mwenyekiti na mwenyeji wa mkutano wa tatu wa dharura wa baraza la mawaziri wa nchi zinazozalisha almasi (ADPA) itakuwa na mkutano wa baraza la mawaziri kesho tarehe 29 julai 2022 katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha.

Waziri wa Madini Dkt Doto Biteko amezungumza hayo leo jijini Arusha katika mkutano na wanahabari wakati akieleza nia na dhumuni la mkutano huo.

Waziri Dkt Biteko amesema kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha kamati ya wataalamu ambacho kinakaa Leo kupitia taarifa na nyaraka na kabla ya kuwasilisha kwenye baraza.

"Lengo la mkutano huu pamoja na mambo mengine ni kuidhinisha nyaraka muhimu za ADPA zilizofanyiwa marekebisho ambazo ni katiba, kanuni na miongozo ya umoja huo na kuteua viongozi watatu wa Sekretarieti ambao ni katibu Mtendaji na manaibu wake wawili" - amesema Dkt Biteko.

Dkt Biteko amesema Jumuiya ya wazalishaji wa almasi afrika (ADPA) ilianzishwa kwa mujibi wa azimio la Luanda, Angola mnano  November 2006 na lengo kuu la kuundwa kwa ADPA ni kuzipatia nchi zinazozalisha Almasi Afrika jukwaa la kuzikutanisha nchi zote za Afrika katika kusudi moja la kuhakikisha rasilimali za madini hayo zinanufaisha nchi wanachama pia zinapokutana nchi wanachama zinazhirikiana uzoefu na ushirikiano katika nyanja anuwai za Sekta ya almasi.

Aidha Dkt Biteko amesema kuwa katika kipindi hicho chote Tanzania ni mwenyeji wa Jumuiya hiyo imekuwa ni heshima kubwa kwa kuwajibika kwa ajili ya marndeleo ya nchi, hususani katika usimamizi wa madini ya almasi ambapo kama ilivyoahidi nchi ya Tanzania Wakati ikikabidhiwa nafasi hiyo imewezesha kupitiwa Kwa mfumo wa jumuiya hiyo ikiwepo marekebisho ya katiba na kanuni pia miongozo mbalimbali ya jumuiya.

Aidha Dkt Biteko amebainisha kuwa Kama nchi imejifunza zaidi kuhusu usimamizi wa sekta hususani Kwa madini ya Almasi ambapo pia nchi wanachama na hata wasio wanachama walipata nafasi ya kuja kujifunza kuhusu namna Tanzania ilivyofabikiwa kuwaendeleza wachimbaji wadogo wakiwepo wa madini ya almasi na madini ya dhahabu na namna ambavyo Serikali ilivyoweza kusimamia mifumo inayohusisha mnyororo mzima wa shughuli za madini.