Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu ya Msingi wa Afrika Kusini Mhe. Matsie Angelina Motshekga jijini Dar es Salam.

Waziri Motshekga yuko nchini kwa mualiko wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya utiaji saini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa maendeleo ya elimu ya msingi ikiwa ni pamoja na ufundishaji wa kiswahili katika shule za msingi za Afrika Kusini.

Hati hiyo ya makubaliano inatarajiwa kusainiwa tarehe 7, 2022 katika maadhimisho ya siku ya kiswahili Duniani

Waziri Mkenda amesema kupitia hati hiyo ya makubaliano kiswahili kinakwenda kupanuka kwa kufundishawa nchini Afrika Kusini na hivyo kuimarisha uhusiano wa muda mrefu wa kiundugu uliopo baina ya nchi hizo mbili

Naye Mhe. Motshekga amesema wananchi wa Afrika Kusini wanafuraha sana baada kusikia nchi ya Tanzania imekubali kufundisha kiswahili nchini humo na kuwa wako tayari kupokea wataalamu wa kiswahili kuja kufundisha.

Nae Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini Mhe. Meja Jenerali Gaudence Milanzi ( MSt) amesema wamefarijika kwa hatua iliyofikiwa na Wizara hizo mbili na kutoa wito kwa watanzania kuchangamkia fursa adhimu ya kufundisha kiswahili Afrika kusini.

Viongozi hao wamekubaliana baada ya kusainiwa kwa hati hiyo timu za wataalamu kutoka nchi zote mbili zitakaa na kuweka mpango kazi ili utekelezaji uanze mara moja