Mgombea pekee wa nafasi ya urais Yanga, Injinia Hersi Said amechaguliwa na wanachama baada ya kuridhia kwa kupiga kura za ndio.


Mwenyekiti Kamati ya uchaguzi Mchungahela kwa mujibu wa ibara ya 23(9) ya kanuni za uchaguzi ya shirikisho la soka Tanzania TFF inasema mgombea akiwa mmoja mkutano Mkuu unapitisha azimio la mgombea kuwa Rais.


"Wajumbe mnaridhia Hersi Said kuwa Rais wa Klabu ya Yanga," amesema Mchungahela huku wajumbe wakiitikia ndio.


Mchungahela amerudia mara tatu kauli hiyo wajumbe wakionekana kumkubali.


Baada ya kupiga kura hizo za wazi za ndio Mchungahela amemtangaza rasmi kuwa Rais wa klabu hiyo.


Wajumbe hao walianza kuimba Hersi Hersi ikamlazimu kupanda jukwani na kuwapungia mikono ikiwa ishara ya shukrani kwa kumuamini.