Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA),  limewasilisha rasmi serikalini malalamiko yake ya kutoridhishwa na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma.

Malalamiko.hayo yamewasilishwa serikalini kwa njia ya maandishi.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, viongozi wa TUCTA wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo Tumaini Nyamuhokya
wamesema, wameamua kuwasilisha malalamiko hayo baada ya kuwepo kwa sintofahamu katika nyongeza ya mishahara waliyolipwa watumishi mwezi huu wa Julai.

Wameongeza kuwa katika nyongeza hiyo baadhi ya kada na taasisi za umma hazijaguswa.

Shirikisho hilo la Vyama vya Wafanyazi Nchini limependekeza kuwa nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma ni vema ikazingatia zaidi asilimia kuliko kiwango cha fedha.

Mei 14 mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza ongezeko la mishahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 23.3.

Hata hivyo, baadhi ya wafanyakazi wamelalamikia kiasi cha fedha walichoongezwa, hatua ambayo imeilazimu TUCTA kuwasilisha rasmi serikali malalamiko hayo.