Jeshi la Urusi limeushambulia mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine l, baada ya Moscow kutangaza kuwa inapanua malengo yake ya kivita. 

Mashambulizi dhidi ya mji huo wa Kharkiv yamekuja baada ya kumalizika kwa siku 10 za matenegenezo ya bomba la kusafirisha gesi ya Urusi kwenda Ulaya, ambayo yalizusha hofu ya kuzimwa kabisaa kwa bomba hilo.

 Gavana wa Kharkiv Oleg Synegubov, amesema kupitia mtandao wa kijamii, kwamba watu wawili wameuawa na 19 kujeruhiwa. Mshauri wa rais Mykhaylo Podolyak, amesema kumekuwa pia na uharibifu kwenye msikiti mjini Kharkiv

Mataifa ya magharibi yameimarisha ugavi wa silaha kwa Ukraine lakini Rais Volodymyr Zelenskiy ameomba silaha zaidi na uwasilishaji wa haraka. 

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alisema jana kuwa Washington itatuma mifumo minne zaidi ya makombora inayojulikana kama HIMARS, ambayo imeongeza pakubwa uwezo wa Ukraine kwenye uwanja wa mapambano. Uingereza pia imetangaza kuipatia Ukraine zaidi ya silaha 1,600 za kushambulia vifaru na silaha nyingine ndogondogo