Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi Yanga SC Malangwe Mchungahela ametangaza Arafat Haji kuwa ndio mshindi wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Yanga kwa kura 545 dhidi ya Suma Mwaitenda aliyepata kura 234.

Kwa mujibu wa kura zilizopigwa nafasi ya wajumbe watano wa kamati ya Utendaji walioshinda ni Yanga Makaga, Seif Gulamali, Rogers Gumbo, Munir Seleman na Alexander Ngai.

Wajumbe na makamu wa Rais sasa wanaenda kuungana na Rais wa club Injinia Hersi ambaye mapema alipitishwa bila kupingwa kuwa Rais wa club hadi 2030.