Na .WAF-Dodoma
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu June 24,2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Zabulon Yoti kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu Afya.
Miongoni mwa mambo walioyajadili ni pamoja na uzinduzi wa utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 katika Mkoa wa Manyara ambapo watashiriki viongozi kutoka Wizara ya Afya pamoja na Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika la Afya Duniani na wananchi kwa ujumla.
Aidha Dkt. Yoti ameahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kupambana na ugonjwa wa Polio na UVIKO-19 pamoja na kutoa ushauri Serikali iendelee kuhuisha mara kwa mara Mpango Mkakati wa utoaji wa chanjo nchini