Vikosi vya Urusi vimeharibu njia zote za kuwaokoa raia kutoka mji wa Sieverodonetsk ulioko mashariki mwa Ukraine, baada ya kuharibu daraja pekee lililosalia linalo unganisha mji huo na upande mwingine wa mto.
Hayo ni kulingana na maafisa wa Ukraine.Jeshi la Ukraine limesema kwamba vikosi vya Urusi vimekuwa vikijaribu kupiga hatua kudhibiti baadhi ya maeneo ya kati ya mji huo.
Gavana wa jimbo la Luhansk Serhiy Gaidai amesema takriban raia 500 wangali mjini humo kwenye maeneo ya kiwanda cha kemikali Azot, miongoni mwao wakiwa watoto 40.Eneo hilo la viwandani lilikumbwa na mashambulizi makali kutoka Urusi.