Urusi imesema vikosi vyake vimechukua udhibiti kamili wa mji wa mashariki mwa Ukraine wa Sieverodonetsk. 

Wizara yake ya Ulinzi imesema vikosi vyao vimechukua pia udhibiti wa mji jirani wa Borivske. 

Hapo awali, Ukraine ilisema vikosi vyao vilijiondoa Sieverodonetsk baada ya siku kadhaa za mapigano makali. Kwa kuukamata Sieverodonetsk, inamaanisha Urusi sasa inadhibiti takriban eneo zima la Luhansk Oblast katika mkoa wa Donbas. 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekiri kuwa vita hivyo vimefikia kipindi kigumu sana, lakini ameapa kwamba mashambulizi ya Urusi hayatavunja nia ya Waukraine.