Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa wakiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi wamekutana na Balozi wa Marekani hapa nchini leo Juni 8, 2022 wamekutana jijini Dar es salaam na kujadili masuala mbali mbali ya sekta za ikiwa ni pa moja na ujio wa msanii mashuhuri wa uchoraji ,Ashley Collins hapa nchini.

Wakizungumza katika  kikao hicho ambacho Mhe. Balozi  wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright ameambatana na Afisa Uhusiano wa Ubalozi huo, James Rodriguez wamejadili pia ujio wa Timu ya wachezaji nguli wanawake ya mchezo wa kikapu wa ligi  ya NBA nchini Marekani  hapa nchini ambao watakuja Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wachezaji wanawake wa mchezo huo hapa nchini.

Mhe. Mchengerwa amesema viongozi hao wamekubaliana  kuendeleza  malengo ya Royal Tour kwa kushirikiana zaidi  kwenye kuendeleza sekta  za sanaa na michezo ikiwemo kuendeleza  filamu za hapa nchini za “Swahiliwood” ili ziwe  katika  kiwango cha kimataifa kama zile za nchini Marekani kwa kupata walaam ambao watasaidia katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandaa miswada (script)

Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na maeneo ya kipekee ya kuchezea  filamu ambazo zingeweza  kuwa bora na kusisitiza kuwa ni azma ya serikali kujenga mazingira  wezeshi ikiwa ni pamoja na kuangalia kodi mbalimbali ili kuwavutia wageni kuja  kurekodia  hapa nchini.

Aidha amesema eneo jingine ambalo limejadiliwa ni pamoja na kutoa mafunzo maalum katika eneo la haki miliki na hakishiriki kwa kazi mbalimbali za wasanii ikiwa ni pamoja na tuzo za muziki na Kwa upande mwingine amesema wamejadili namna ya kushirikisha wataalam kwenye program maalum ya kuibua vipaji vya wasanii na wanamichezo ya mtaa kwa mtaa.