Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali inampango wa kuanzisha utaratibu wa kutoza ada ya Sh1,000 hadi Sh3,000 kwenye ada ya matumizi ya king’amuzi kulingana na kiwango cha matumizi.

Kauli hiyo ameitoa  Juni 14, 2022 jijini Dodoma, wakati akiwasilisha akiwasilisha mapendekezo ya serikali ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23 huku akidai hatua hiyo inalenga kuongeza mapato ya Serikali.

Waziri huyo pia amependekeza kuanzishwa tozo ya asilimia 1.5 kwenye vifaa vinavyotumika kuzalisha, kusambaza, kudurufu na kutunza kazi za sanaa, uandishi na ubunifu mwingine kama vile muziki, filamu, vitabu, picha na aina nyingine za kazi za ubunifu.

“Vifaa hivi ni Radio/ TV set enabling recording; Analogue audio recorders; Analogue video recorders; CD/DVD Copier; Digital Jukebox na MP 3 Player. Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh9.6 bilioni,”

Pia amesema Serikali kupitia  Shirika la Viwango Tanzania inampango wa kupunguza tozo ya kuthibitisha ubora wa shehena (Batch Certification Fee) za sukari zinazoingizwa nchini kutoka sh 6 kwa kilo hadi 2.5 Lengo la hatua hiyo  kupunguza gharama kwa waingizwaji wa bidhaa hiyo  na kutoa unafuu kwa wananchi.

Dk Mwigulu amependekeza kuondoa tozo ya vibali vya ukaazi kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka nchi ya Msumbiji.

Amesema lengo la hatua hiyo ni kutekeleza matakwa ya makubaliano kati ya nchi hiyo na Tanzania kuondoleana tozo hizo ambapo Msumbiji imeshaanza kutekeleza makubaliano hayo.

Hayo amebainisha Juni 14, Dodoma, wakati akiwasilisha akiwasilisha bungeni mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23.

“Mwaka wa fedha 2021/22 Serikali ilipitisha uamuzi wa kuondoa ada ya kibali cha kuingian nchini (VISA/PASS FEE) kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka nchi ya Msumbiji kwa ajili ya Mpango wa kubadilishana wanafunzi wa elimu ya juu baina ya Tanzania na Msumbiji (TAMOSE),”amesema