KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Prof.Riziki Shemdoe ameridhia kufanyika kwa uhamisho watumishi 1,048 wa kubadilisha vituo vya kazi pekee. Watumishi hao ni wale walioomba uhamisho kuanzia Mwezi Februari-Mei,2022.
 
Aidha amewakumbusha watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa uhamisho wa kwenye Halmashauri za Majiji, Manispaa na Miji umesitishwa mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo. 

Amewataka watumishi waliopata uhamisho huu kusubiria barua kwenye Halmashauri zao na sio kufika Ofisi ya Rais-TAMISEMI kufuata barua hizo.