Waumini wa dini ya Kiislamu nchini leo wanaungana na wenzao wa mataifa mbalimbali kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitr.

Sikukuu ya Eid El Fitr inasherehekewa baada ya kukamilika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambao ni moja kati ya nguzo tano za Uislamu

Kitaifa swala ya Eid imeswaliwa katika Msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Swala hiyo ya Eid El Fitr itafuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.