Wahadzabe Manyara kupatiwa Nyama zoezi la Sensa mwaka 2022.
Na John Walter-Manyara
Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere amewataka Wananchi mkoani humo kutoa ushirikiano kwenye zoezi la Sensa ya watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu.
Amesema wataandaa Nyama ya kutosha kwa ajili ya jamii ya wahadzabe wanaofanya shughuli za uwindaji ili zoezi la uhesabuji watu linapofanyika wawepo katika nyumba zao.
"Niwahakikishie Wahadzabe,zoezi la Sensa ya watu na tumewaandalia nayama ya kutosha" alisema Makongoro
Amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi katika maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi mkoani humo zilizofanyika mjini Babati.
Mbunge wa Jimbo la Babati mjini (Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo mheshimiwa Paulina Gekul, amesema Sensa ni Muhimu kwa maendeleo ya Taifa hivyo ni muhimu watu wote kushiriki kikamilifu.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alitangaza zoezi la Sensa ya watu na Makazi kufanyika Agosti 23,2022 ikiwa na kauli mbiu isemayo 'Sensa kwa Maendeleo, Jiandae kuhesabiwa".
Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS), ipo kwenye maandalizi ya kufanya Sensa hiyo.
Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012, hivyo Sensa ya mwaka 2022 itakuwa ni sensa ya Sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.