UTANGULIZI

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari (Sayansi miaka mitatu). Waombaji wa mafunzo haya ni wahitimu wa Kidato cha NNE wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.

SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU

Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari (sayansi miaka mitatu) ni wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III.

AINA YA MAFUNZO NA SIFA

Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya mafunzo ya Ualimu, sifa za kujiunga, vyuo vinavyotoa mafunzo hayo na muda wa mafunzo.

==>>BOFYA HAPA KUPAKUA FOMU, VIGEZO NA KUTUMA MAOMBI .

 

  • Mwisho wa kutuma maombi kwa Mafunzo ya Ualimu ni tarehe 31/05/2022.