Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam hivi sasa inaendelea kusikiliza maombi ya wabunge 19 wa viti maalum ambao walikuwa wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na baadaye kufukuzwa uanachama.

Wabunge hao walipeleka maombi yao Makahama Kuu kupinga kufukuzwa uanachama na chama hicho.

Shauri hilo la wabunge 19 waliokuwa wanachama wa CHADEMA linasikilizwa na Jaji John Mgeta.

Mapema hii leo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKt.Tulia Ackson aliliambia bunge kuwa kwa sasa hawezi kutamka kuwa viti 19 vya wabunge hao vipo wazi, kwa kuwa suala hilo lipo mahakamani.