Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesisitiza udharura wa wa kuzuia kujiri vita vya nyuklia. Moscow imeeleza hayo kutokana na wasiwasi juu ya uwezekano wa kushuhudiwa vita vya nyuklia duniani.

Sambamba na kutumia siku ya 67 tangu kuanza mashambulizi ya nchi yake dhidi ya Ukraine, Sergei Lavrov amesisitiza kwamba mapigano   ya silaha baina ya madola yanayomiliki silaha za nyuklia yanapaswa kuepukwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameeleza kuwa, nchi wanachama wa Muungano wa Kiijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) hazisiti kufanya lolote ili kuzuia makubaliano ya kisiasa kati ya Moscow na Kiev, na ameitaka NATO na Marekani kuacha kuipatia silaha na zana za kijeshi serikali ya Ukraine.

Baada ya viongozi wa maeneo yaliyojitangazia uhuru ya Donetsk na Luhansk huko mashariki ya Ukraine kuiomba Russia iwatumie misaada ya kijeshi kwa mujibu wa makubaliano ya ushirikiano kati yao,  Rais Vladimir Putin wa Russia tarehe 24 Februari alitangaza kuanza operesheni maalumu ya kijeshi nchini Ukraine.

Marekani na watifaki wake wameiwekea Russia vikwazo kutokana na Moscow kuwaunga mkono raia  wa Russia huko mashariki mwa Ukraine na pia kufuatia hatua ya Russia ya kutangaza kutambua rasmi uhuru wa aeneo ya Donetsk na Luhans. Russia imetangaza mara kadhaa kwamba haitaruhusu nchi hiyo ikabiliwe na vitisho kupitia Ukraine.