Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameelekeza Jeshi la Polisi kuanza Mara moja msako wa kuwakamata Watuhumiwa wa Wizi na unyang'anyi kwa kutumia silaha maarufu Kama Panya road na kuwachukulia hatua Kali za kisheria.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo Kufuatia taharuki iliyoibuka Miongoni mwa Wananchi Baada ya kutokea kwa matukio ya uhalifi maeneo mbalimbali ikiwemo Tabata, Chanika, Zingiziwa na kunduchi ikihusisha vijana wa Kati ya miaka 13 Hadi 21.

Hali hiyo ndio imemlazimu RC Makalla kuitisha kikao kazi Cha kukabiliana na uhalifu huo kikihusisha  Kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa, Wilaya, Wakuu wa usalama, Makamanda wa Wilaya zote za kipolisi, Wakuu wa Vituo vya Polisi na Maafisa Polisi Jamii wa Kata na kuwapatia maelekezo.

Miongoni mwa maelekezo aliyotoa RC Makalla ni pamoja na Kamati za ulinzi na usalama ngazi ya Wilaya kufanya kikao na Wenyeviti wote wa Mitaa husika agenda ikiwa kudhibiti uhalifu.

Aidha RC Makalla ameelekeza OCD, Wakuu wa Vituo vya Polisi na Polisi Jamii kuongeza doria za Mitaa kwa kutumia magari na Pikipiki ambapo pia ameelekeza Kila Mkoa wa kipolisi kutoa taarifa ya mwenendo wa Operesheni kila siku.

Hata hivyo RC Makalla ameelekeza Jeshi la Polisi kuanza msako wa kuwakamata wanunuzi wa Mali za Wizi huku akiwataka Wakuu wa Wilaya kuweka utaratibu mzuri wa kuanza kuwatumia Askari Mgambo katika kuongezea Nguvu Jeshi la Polisi.

Pamoja na hayo RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi kuondoa hofu kwakuwa Serikali kupitia Jeshi la Polisi limejipanga kudhibiti uhalifu wowote.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam Jumanne Muliro amesema Jeshi Hilo limejipanga kutekeleza maelekezo ya RC Makalla ambapo amesema tayari wanawashikilia Watuhumiwa mbalimbali.