Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeridhia wabunge 19 wa viti maalum waliovuliwa uanachama wao na CHADEMA kuendelea na ubunge wao mpaka maombi ya kibali cha kufungua kesi ya kupinga uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA ulioridhiwa na wajumbe wa baraza kuu utakaposikilizwa na kutokewa uamuzi. 

Maombi hayo ya zuio la muda la ubunge wao, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), yamesikilizwa leo Jumatatu, Mei 16, 2022 mbele ya Jaji John Mgetta .