Baraza Kuu la CHADEMA usiku wa kuamkia alhamisi (Mei 12, 2022) limezitupilia mbali rufaa za Halima Mdee na wenzake 18 za kupinga kufukuzwa uanachama na kamati kuu ya chama

Baraza hilo limeunga mkono uamuzi wa kamati kuu ya chama wa kuwafukuza uanachama Halima Mdee na wenzake kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge wa viti maalumu bila kupata baraka za chama

Akizungumza mara baada kumalizika kwa mkutano wa Baraza hilo Halima Mdee amesema “Kilichofanyika ni Uhuni, hata Mbowe (Freeman) mwenyewe anajua”

Mkurugenzi wa mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema Baada ya uamuzi wa Baraza Kuu, amesema “Katibu Mkuu ataandika barua kumuarifu Spika kuwa suala lao limehitimishwa; tutamwachia spika afanye uamuzi kama alivyosema anasubiri Rufaa zao’.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amesema hakuna uhuni uliofanyika na kura zimepigwa huku wakina Halima (Mdee) wakishuhudia.