Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila amesema, kukamilika na kuzinduliwa kwa barabara ya Nyahua hadi Chaya kutafungua na kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji katika mikoa ya Singida na Tabora pamoja na mikoa jirani.

Akisoma taarifa ya ujenzi kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa barabara hiyo, Mhandisi Mativila amesema barabara hiyo iliyojengwa kwa kiwango cha lami ina urefu wa kilomita 85.4.

Amesema barabara hiyo ya Nyahua hadi Chaya ina makaravati makubwa 32 na madogo 60.

Barabara hiyo imejengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 123 na ujenzi wake umechukua muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2017 hadi 2021.