Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zimeanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 4 Mei 2022. Pamoja na kutambua bei hizo, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:-


(a) Bei za rejareja za petroli ni Shilingi 3,148 kwa lita kwa Dar es Salaam, Shilingi 3,161 kwa lita kwa Tanga na Shilingi 3,177 kwa lita kwa Mtwara;
(b) Bei za rejareja za dizeli ni Shilingi 3,258 kwa lita kwa Dar es Salaam, Shilingi 3,264 kwa lita kwa Tanga na Shilingi 3,309 kwa lita kwa Mtwara;
(c) Bei za rejareja za mafuta ya taa ni Shilingi 3,112 kwa lita kwa Dar es Salaam na bei za bidhaa hiyo kwa mikoa yote nchini zimekokotolewa kulingana na gharama za kupokelea mafuta hayo kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka miji husika.
(d) Mabadiliko ya bei yanatokana na ongezeko la bei za mafuta katika soko la dunia zinazochangia takribani asilimia 93 ya ongezeko la bei hizo na gharama za uagizaji (premium) ambazo zinachangia takribani asilimia 4. Vilevile, bei za mafuta hapa nchini zina uwiano na bei za bidhaa hizo katika nchi jirani.

==>>Bofya Hapa Kupakua PDF Yenye Bei za Mikoa Yote.