Na Lucas Raphael,Tabora
Zaidi ya watoto 600,000 mkoani Tabora wanatarajia kupatiwa chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 katika kampeni ya kitaifa inayotarajiwa kuzinduliwa aprili 28 mwaka huu nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batrida Buriani  katika kikao cha kamati ya Afya ya msingi ngazi ya mkoa iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mtemi Isike  Mwanakiyungi mkoani hapa.

Alisema kwamba watoto 619,812 watapatiwa chanjo ya polia ilikuweza kuzuia ugonjwa wa kupoonza kwa watoto walio chini ya miaka 5 .

Alisema kwamba mkoa wa Tabora tayari umeshapokea dozi 712,780 za chanjo ya Matone ya polio ambazo tayari zimesambazwa katika halmashauri zote za mkoa huo.

Alisema kwamba kampeni hiyo ya chanjo  itafanyika kwa kupita nyumba kwa nyumba ,vituo vya kutolea huduma za afya ,maeneo maalum yenye mikusanyiko ya watu wengi .

Balozi Dkt Batrida alitaja maeneo hayo kuwa ni nyumba za Ibada Shule za awali,vituo vya kulelea watoto wadogo muda wa mchana,makao ya watoto ,Stedi za mabasi ,masoko na minadani.

Mkuu huyo wa mkoa wa Tabora alisema kwamba maandalizi yote ya utekelezaji wa kampeni hiyo yameshakamilika katika ngazi zote , kuanzia ngazi ya mkoa,Halmashauri na kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Alisema kwamba lengo ni kuhakikisha watoto waliolengwa wanapatiwa chanjo ya kukingwa na ugonjwa wa polio wanapata huduma ya chanjo.

Mnamo Februari 17 mwaka huu katika nchini ya Malawi ilitolewa taarifa ya mgonjwa huyo wa polio alipatikana katika mji mkuu wa Malawi wa Lilongwe .

Kutokana na mwingiliano wa wananchi baina ya Tanzania na Malawi na tathimili iliyofanyika na wizara ya Afya na Shirika la Afya Duniani (WHO)ambapo  Tanzania ilionekana ni miongoni mwa nchi zilizo katika hatari kubwa kupata maambukizi ya ugonjwa wa Polio endapo hatua madhubuti hazitachukuliwa .