Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO amewaambia wananchi Kuwa hali ya ulinzi na usalama katika jiji la Arusha na Mkoa ni  shwari kuelekea uzinduzi wa filam ya The Royal Tour.

Kamanda Masejo amesema kuwa Kuelekea uzinduzi wa filamu maalum ya The Royal Tour Tanzania Kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo limejianga vyema kuhakikisha dunia inashuhudia uzinguzi huo wa filamu ya the Royal Tour itakayo
fanyika siku ya kesho 28.04.2022 katika kituo Cha kimataifa Cha Mikutano Arusha AICC.

Kamanda Masejo amesema kama ilivyo desturi ya wakazi wa jiji la Arusha kuwa wakarimu kwa wageni basi vyema wakaionyesha dunia ukarimu huo na kuionyesha dunia kuwa Arusha ni kitovu Cha utalii.