Ujerumani inatarajia kuidhinisha uamuzi wa kuipelekea Ukraine vifaru aina ya Leopard vinavyoweza kujihami dhidi ya mashambulio ya ndege. 

Mbunge mwandamizi wa chama cha waliberali, FDP, Johennes Vogel, amethibitisha kwamba Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Christine Lambrecht, anatarajiwa kutoa maelezo kamili kwenye mkutano wa nchi 40 unaofanyika kwenye mji wa Ramstein, wa kusini magharibi mwa Ujerumani.

 Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ambaye amekuwa analaumiwa kwa kusita kuipelekea Ukraine silaha nzito sasa ameahidi kuwa Ujerumani itaipeleka nchi hiyo silaha za ulinzi wa anga na za kujihami dhidi ya vifaru.