Chuo Kikuu Kishiriki Cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) kinatangaza nafasi za masomo kwa mwaka 2022/2023 katika ngazi ya Cheti na Diploma zinazotolewa na Taasisi Tanzu ya Masoka Professionals Training Institute iliyopo Moshi Mjini, Kozi hizi zitaanza Mwezi Mei, 2022.
Nafasi ni kwa kozi zifuatazo:
1. Business Administration
2. Community Development
SIFA ZA MWOMBAJI
Kozi za Cheti: Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne awe na ufaulu wa alama D nne na kuendelea isipokuwa somo la Dini.
Diploma: Mwombaji awe amemaliza kidato cha sita na awe na Principal Pass moja na subsidiary moja isipokuwa somo la Dini AU awe amehitimu cheti (astashahada) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.
Chuo pia kinatangaza nafasi za ufadhili wa nusu ada kwa waombaji wanaotoka katika sharika zote za KKKT Dayosisi ya kaskazini. Hivyo wote wenye sifa wanahimizwa kufika kwa wachungaji wao ili kusajiliwa katika mpango huu maalumu.
Maombi yanaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia smmuco.osim.cloud/apply
FOMU ZINAPATIKANA SEHEMU ZIFUATAZO
1. Tovuti ya Chuo: www.smmuco.ac.tz
2. Chuoni - Moshi Mjini.
3. KKKT Christian Bookshop Moshi Mjini – mkabala na stendi kuu ya mabasi
4. Ofisi za Sharika zote za KKKT Dayosisi ya kaskazini.
Kwa maelezo zaidi: Piga simu namba: 0653422928, 0756512757, 0786862089, 0756029652
Pia Chuo kina kozi zingine zitazotolewa Mwezi Septemba ambazo ni:
SHAHADA
1. Bachelor of Arts in Community Development
2. Bachelor of Accounting and Finance
3. Bachelor of Arts with Education
ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA)
1. Law
2. Tour guiding and Tourism
3. Information Technology
4. Human Resource Management
5. Journalism
6. Accountancy
7. Business Administration
8. Procurement and Supply
9. Community Development
10. Records and Archives Management
NYOTE MNAKARIBISHWA