Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 02 – 21 Machi, 2022 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. 

Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Data base) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.


Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazijachukuliwa na Wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.


Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.


Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

 

==>>BOFYA HAPA KUTAZAMA MAJINA

____

==>> BOFYA HAPA KUTAZAMA NAFASI MBALIMBALI ZA KAZI