Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) imepata kibali cha ajira za Watumishi wa Kada za Afya 7,612 kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na Ualimu 9,800 wa Shule za Msingi na Sekondari watakaofanya kazi chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.


Hivyo, wahitimu kutoka kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kuanzia tarehe 20 Aprili - 04 Mei, 2022. Nafasi za ajira zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree).

==>>BOFYA HAPA  kupakua PDF/ Kujua zaidi na Kutuma Maombi .

________

Tangazo hili linawahusu wahitimu wa Kozi za Ualimu kuanzia
mwaka 2015 hadi mwaka 2021.