Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amempongeza Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa jitahada zake za kutangaza vivutio mbalimbali nchini kwa kuzindua makala maalum ya kuhamasisha utalii ijulikanayo kama "ROYAL TOUR" ambayo uzinduzi wake umefanyika jana Aprili 18, 2022 nchini Marekani.

Spika Dkt. Tulia ameyasema hayo leo Aprili 19, 2022 Bungeni Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa saba wa Bunge la bajeti unaoendelea.

"Sisi kama Bunge, tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa hatua anazozichukua kwenye hili eneo la kuongeza watalii. Kwakuwa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii itakuja hapa Bungeni baadae basi ni muhimu kila Mbunge kufuatilia mambo yanayoendelea huko ili kama kutakuwa na lolote la kuishauri Serikali itakuwa rahisi zaidi baada ya kujua hatua mbalimbali ambazo zitakuwa zimeshachukuliwa na zile ambazo tutakuwa tunatamani ziongezeke" amesisitiza Spika. Dkt. Tulia