Aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki amefariki akiwa na umri wa miaka 90. Rais Uhuru Kenyata ametangaza muda mfupi uliopita kupitia runinga mbalimbali nchini Kenya.

Kibaki alikuwa rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya kutoka mwaka 2002 hadi 2013. Rais Uhuru Kenyatta amesema kiongozi huyo wa zamani wa taifa ataandaliwa mazishi ya kitaifa.

Uhuru ametangaza kuwa Kibaki amefariki usiku wa siku ya Alhamisi.Uhuru anamuomboleza mtangulizi wake kama kiongozi ambaye alileta ukuaji wa kiuchumi , demokrasia na kuimarisha hali ya uchumi ya Wakenya.

Amesema kwamba benderazote katika majumba ya umma , wizara na balozi zote duniani zitasalia nusu mlingoti hadi pale atakapozikwa.