Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge yaomba Bil 148 kwenye Bajeti 2022/2023
Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake imeomba bunge kuidhisha jumla ya shilingi bilioni mia moja arobaini na nane, milioni mia nane tisini na mbili, laki tano na elfu hamsini na tatu (148,892,553,000) kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Kati ya fedha hizo shilingi bilioni mia moja na moja, milioni mia tatu na sitini na tano, laki tatu na elfu tisini na nane (101,365,398,000) ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi Bilioni Arobaini na Saba, Milioni Mia Tano Ishirini na Saba, Laki Moja na Elfu Hamsini na Tano (47,527,155,000) ni kwa ajili ya maendeleo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliomba Bunge liidhinishe jumla ya shilingi 132,728,638,000.00 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo kati ya fedha hizo shilingi 127,328,638,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 5,400,000,000.00 ni kwa ajili ya Maendeleo.
Waziri Mkuu alikuwa akiwasilisha Bungeni jijini Dodoma Mapitio na Mwelekeo wa kazi za Serikali pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.