Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Bara Philip Mangula amesema, licha ya kung’atuka katika nafasi hiyo ataendelea kufanya kazi za chama hicho kwa uadilifu.

Amesema amekua kiongozi ndani ya CCM kwa muda mrefu na sssa anaona wakati umefika kuwaachia wengine, ili na yeye aendelea na shughuli nyingine za kukiimarisha chama.

Mangula amesema safu ya uongozi iliyopatikana kwa sasa ndani ya CCM ni nzuri, na ni matumaini yake itafanya kazi yake vizuri ya kukuiimarisha chama na kuwatumikia Wananchi.

Mangula alikuwa akizungumza katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM mkoani Dodoma mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM Tanzania Bara ambapo Abdulrahman Kinanna amepata asilimia mia moja ya kura zote zilizopigwa.