Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akizungumza na Waandishi wa habari leo Aprili 4, 2022 katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo Katibu Nenelwa alisema baada ya maboresho ya Studio ya Bunge, Kamati ya Uongozi ya Bunge imeridhia Vikao vya Bunge vitaanza kurushwa live kuanzia kesho tarehe 5 Aprili, 2022 wakati wa Mkutano wa 7 wa Bunge ambao ni mahsusi kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya Serikali.