Aliyekuwa Spika wa Bunge Job Ndugai, leo amehudhuria kikao cha kwanza cha bunge la bajeti kwa mwaka 2022 hadi 2023 tangu ajiuzulu.

Job Ndugai, alijiuzulu wadhifa huo mnamo Januari 6, 2022, kwa maelezo ya kwamba alifanya hivyo kwa ajili ya maslahi ya chama chake na Taifa, baada ya kuonekana akikejeli mkopo wa trilioni 1.3 uliochukuliwa na serikali.

Kupitia mitandao ya kijamii hivi karibuni, watu wengi walikuwa wakihoji ni wapi alipo mbunge huyo wa Kongwa, baada ya kutoonekana kwa muda.