Jeshi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Latifa Bakari (33) mkazi wa Mabibo mkoani Dar es Salaam, kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa mdogo wake aliyekuwa na umri wa miaka miwili na miezi minne.

Mtuhumiwa huyo aliachiwa mtoto huyo na mdogo wake ili amlee na tarehe 5 mwezi huu alifanya mauaji hayo baada ya kumpiga kupita kiasi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Muliro Jumanne amesema baada ya kubaini kuwa mtoto huyo amefariki dunia kutokana na kipigo, tarehe 6 mwezi huu mtuhumiwa huyo aliuchukua mwili wake na kuukunja na kuuweka kwenye ndoo ya plastiki na kisha kuudumbukiza kwenye kiroba na kwenda kuutupa eneo la River Side Ubungo.

Baaba ya majirani kutomuona mtoto huyo walitoa taarifa polisi ambao walifanya mahojiano na mtuhumiwa ambaye alikiri kufanya mauaji hayo na kwenda kuwaonesha polisi ulipo mwili wa mtoto huyo.