Shambulio la Urusi katika kituo cha mafunzo cha karibu na mji wa kati wa Ukraine wa Schytomyr ladaiwa kuwauwa wanajeshi 100 wa Ukraine na wengine wa kigeni. 

Taarifa hizo zinatolewa katika kipindi ambacho kwa siku ya pili jeshi la Urusi linaripotiwa kutumia silaha nzito ya kombora la masafa marefu la Kinshal tangu livamie Ukraine.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi, Igor Konashenkov amesema shambulizi hilo lilifanyika katika kituo cha kijeshi cha mkoa wa Mykolaiv. 

Serikali ya Urusi imesema kituo hicho kilikuwa muhimu kwa ajili ya ujazaji wa mafuta kwa mizinga ya Ukraine. Na kadhalika wameripua karakana ya ukarabati wa mizinga hiyo.

Hata hivyo bado haijiwa awazi silaha gani zimetumika katika shambulizi hilo la Schytomyr.