Maafisa wa Ukraine wamekaidi masharti ya Urusi ya kuwataka wanajeshi wa Ukraine walioko katika mji uliozingirwa wa Mariupol waweke chini silaha zao na kusalimu amri, ili wapewe njia salama ya kuondoka katika mji huo wa kimkakati.

 Urusi imekuwa ikiushambulia kwa mabomu mji huo ulio kwenye bahari ya Azov, ikiilenga shule ya sanaa inayowapa hifadhi watu 400, saa chache kabla ya kuahidi kufungua njia mbili kwa wanajeshi wa Ukraine kuondoka. 

Urusi ilikuwa imeipa Ukraine hadi saa kumi na moja alfajir ya leo kuwa imesalimu amri mjini Mariupol, lakini haikusema itafanya nini ikiwa Ukraine itakataa kuheshimu matakwa yake. 

Naibu waziri mkuu wa Ukraine Irina Vereshchuk ameliambi shirika la habari la nchi yake kuwa hawatokubali mazungumzo yoyote yanayohusisha kuweka chini silaha na kunyosha mikono.