Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema njia ya ya kumaliza vita mara moja nchini Ukraine ni kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Rais Vladimir Putin.

"Hatutaki kuishambulia Urusi na hatupangi kushambulia. Mnataka nini kutoka kwetu? Tokeni kwenye ardhi yetu, ”amesema rais wa Ukraine.

Ameongeza kwa akielezea umuhimu wa kufanya mazungumzo mwezi uliopia:

"Njoni tuketi Pamoja. Msiketi umbali wa mita 30, kama alivyofanya wakati rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alipokutana na Putin."