Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu [Kazi Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu] Prof.Joyce Ndalichako amewaelekeza viongozi wa vyama vya wafanyakazi waweze kumaliza makosa ya yasio ya jinai kwa watumishi wa umma katika sehemu zao za kazi

Prof.Ndalichako ameyasema hayo Machi 12,2022 katika ukumbi uliopo Rayal hotel jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa baraza kuu la shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania [TUCTA] ambapo amesema haipaswi kuwekwa ndani watumishi wa umma kwa makosa yasiyo ya jinai kwani pamekuwa na tabia ya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuwaweka ndani watumishi wa umma kwa makosa yasio ya jinai.

Hivyo,amesema makossa ya kiutendaji kwa watumishi yachukuliwe hatua sehemu za kazi.

Aidha,Prof.Ndalichako amewaagiza waajiri wote nchini kuhakikisha vikao vya mabaraza ya wafanyakazi vifanyike kwa mujibu wa matakwa ya kisheria ikiwemo kulipa posho stahiki kwa wafanyakazi Kwa upande wake rais wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania [TUCTA] Tumaini Nyamhokya amesema kuna haja kwa serikali kutekeleza ipasavyo kuwarejesha kazini watumishi wa darasa la saba kwani kuna baadhi ya taasisi zimekuwa zikiwakataa na kuwanyima stahiki zao huku mwenyekiti wa kamati ya wanawake wa shirikisho hilo Rehema Ludanga akibainisha kuwa bado kuna changamoto ya utekelezaji wa sheria ya mkataba wa kazi.