Mangula ang’atuka, Abdulrahman Kinana kuwa mgombea nafasi ya makamu mwenyekiti wa CCM(Bara)
Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) imempendekeza Katibu mkuu wa zamani wa chama hicho, Abdulrahman Kinana kuwa mgombea nafasi ya makamu mwenyekiti (Bara) baada ya aliyekuwa akishika nafasi hiyo, Philip Mangula kung’atuka.
Hayo yamesemwa leo Alhamis Machi 31, 2022 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa NEC uliofanyika chini ya Uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan.