Na.Abel Paul wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishina msadizi wa Polisi ACP Justine Masejo ameviambia vyombo vya habari kuwa tarehe 02.03.2022 muda wa 07:30 mchana huko maeneo ya Ngarenaro katika halmashauriya jijila Arusha askari Polisi walifanikiwa kuwakamata watuhumi wa wawili ambaoni AMANDA THOMAS (22) mkazi wa kwa Morombo na KELVIN THOMAS (27) mkazi wa Ngarenaro wakiwa na nyama Pori ya mnyama Pofu KG150.

Kamanda Masejo amesema kuwa uchunguzi wa awaliwa tukio hili umebaini kuwa watuhumi wahao wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo ya nyara za serikali ambapo uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na askari wanyama Pori ili kubaini mtandao wao.

Ameendelea kusema kuwa Katika tukio jingine tarehe 02.03.2022 muda wa saa 09:30 alasiri huko kata ya RHOTIA tarafa ya mbulumbulu wilaya ya karatu na Mkoa wa Arusha askari Polisi walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili ambao ni PETRO GAUDENCE (57) mkazi wa mbulumbulu na REVOCATUS PROTUS (28) mkazi wa mbulumbulu wa kiwa na lita 570Ltr za Pombe haramu ya moshi (gongo).

ACP Masejo amewambia waandishi kuwa Operesheni kali inaendelea katika wilaya zote ili kubaini wanaofanya biashara hizo, hivyo ni watake baadhi ya watu wanaojihushisha na biashara hizo haramu ya gongo Pamoja na nyara za serikali kuacha mara moja kwani hatuto muonea muhari mtu yeyote anayejihusisha na biashara hizo haramu.

Amesema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea na upelelezi wa matukio nayo na  mara baada ya upelelezi kukamilika majalada hayo yatapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisherai.

Kamanda Masejo ametoa wito kwa kila wananchi kuwa mlinzi na kulinda rasilimali za nchi adhimu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi
juu ya uhalifu na wahalifu wanaohujumu rasilimali za Nchi ili hatua kali za
sheria zichukuliwe dhidi yao.