Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa na Vikosi kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowasilishwa na wananchi hasa kuhusiana na makosa ya uhalifu kwa njia ya mtandao unaotekelezwa na baadhi ya watu wenye nia ovu.

IGP Sirro amesema hayo jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa na Vikosi pamoja na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Makosa ya Mtandao ambapo amewataka kuhakikisha wanapunguza malalamiko yanayotolewa na wananchi kwa kuyafanyiakazi na wahalifu kukamatwa.

Naye Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Wizara ya Habari, Mulembwa Munaku, amesema kuwa, licha ya hatua mbalimbali kuchukuliwa lakini zipo changamoto za uhalifu wa kimtandao ambapo bado wahalifu wanaendelea kuchukuliwa hatua na kudhibitiwa .