Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka Taasisi zote nchini kuhakikisha zinalinda maeneo yake ili kuepuka uvamizi unaoweza kufanywa na wananchi.

Aidha, amesema ni jukumu la kila mmoja aliyepatiwa hati ya umiliki wa ardhi kulinda mipaka ya eneo lake na kwamba si jukumu la serikali kulinda mipaka hiyo.

Pia ameonya maeneo yote ya serikali kuanzia ngazi ya kijiji kulindwa ili yasivamiwe na kusisitiza kuwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi haitakuwa tayari kuwavumilia wale watakaofanya uvamizi na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Waziri Dkt Mabula alisema hayo leo tarehe 24/03/2022 wakati wa kikao na Viongozi wa Mkoa wa Pwani ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu migogoro katika mkoa huo na uamuzi wa Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975
.