Kauli hiyo ameitoa Machi 8, 2022, mkoani Iringa, wakati akizungumza na Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
"Nilipopata mwaliko siku ile ile nimetoka gerezani, nikathibitisha nitakwenda, kamwe sikuruhusu uchungu na maumivu binafsi vinipe upofu na kiburi cha kutokuiona heshima niliyopewa na Rais," amesema Mbowe