Na Lucas Raphael,Tabora
Jeshi la polisi mkoani Tabora linawashikilia watu wanne akiwemo mganga wa kienyeji aliyekuwa akinunua damu kwa shilingi 600,00 ikiwemo  viungo vya binadamu ambavyo ni  sehemu za siri za wanawake na  wanaume kwa ajili ya shughuli za Uganga

Akizungumza na  waandishi wa habari mkoani hapa ofisini kwake jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard  Abwao(ACP)alisema kwamba katika Operesheni ya kukamata watu waliofanya mauaji januari 21 mwaka huu kwa kuumua mwanafunzi wa darasa la nne aliyekuwa anasoma shule ya Msingi Tutuo mwenye umri wa miaka 14 ilifanikiwa katika wilaya ya Sikonge mkoani hapa.

Alisema kwamba baada ya tukio hilo ufuatiliaji ulianza na kufanikiwa kuwakata watu watatau waliotiliwa mashaka katika mahojiano dhidi yao walimtaja mganga anayeusika kununua viungo vya Binadamu .

Alisema kwamba baada ya kukamwatwa kwa mganga huyo wa kienyeji na kufanyiwa mahojiano alikiri kuwa napelekewa viungo vya binadamu ambavyo ni sehemu za sri za mwanamke na sehemu za sri za mwanaume  .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard  Abwao alisendelea kusema kwamba mganga huyo  aliemtaja kwa majina mtu mwengine ambaye jina limehifadhiwa na sehemu anapopatikana ambapo baada ya taarifa hiyo juhudi za kumtafuta zilifanyika hadi kupelekea kukamatwa kwake ambapo alihojiwa na katika mahojiano ya awali amekiri kuhusika katika utendaji wa  matukio ya mauaji  maeneo mbalimbali.

Alisema kwamba baada ya kufanya mauaji huyo uchukua damu kwa kuwachoma na kitu chenye incha kali katika shingo na kuchukua damu inayoruka na kuikinga katika chupa ndogo na kisha damu hiyo huuzwa kiasi cha Tsh 600,000/=.

Kamanda huyo wa polisi aliongeze kusema kwamba mtu huyo uchukua  baadhi ya viungo vya miili yao ambavyo huwa wanapeleka kwa waganga wa kienyeji ambao huwa ndio wanaowaagiza na kisha kuwalipa fedha kulingana na makubaliano.

Hata hivyo katika mahojiano hayo mtuhumiwa huyo amewataja watu wengine ambao anashirikiana nao katika utekelezaji wa mauaji hayo.

Alisema kwamba mpaka sasa watuhumiwa wanne tayari wamekamatwa na upelelezi unaendelea ili kufikia lengo la kuukamata mtandao wote wa watu wanaohusika na mauaji ambapo  majina yao yamehifadhi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.