Na.WAF,Mara
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hali ya UViKO-19 nchini katika kipindi cha tarehe 29 Januari hadi 4 Februari, 2022, jumla ya 6,938 walipimwa na watu 206 walithibitika kuwa na Virusi vya Corona ndani ya wiki moja.

Waziri Ummy ameyasema hayo jana  wakati ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwl.J.K Nyerere Mkoani Mara.

Amesema wagonjwa wapya 71 walilazwa, kati ya hao asilimia 97% walikuwa hawajachanjwa.Na kwa siku ya tarehe 4 Februari, wagonjwa mahututi 11 waliripotiwa na wote sawa na 100% hawakuwa wamepata chanjo dhidi ya UVIKO-19.

Aidha, amesema wagonjwa watatu (3) wameripotiwa kuwa mahututi na wote (100%) hawajachanjwa.

Kwa upande wa vifo Waziri Ummy amesema kwa tarehe 29 Januari hadi 4 Februari,2022, Jumla ya vifo vitatu (3) vimeripotiwa  kutoka mikoa ya Dodoma (1), Morogoro (1) na Manyara (1), vifo vyote (100%) vilivyoripotiwa vilikuwa vya wagonjwa ambao hawakuchanjwa.