Adeladius Makwega,WUSM-Dodoma.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Pauline Gekul Februari 3, 2022 amekutana na menejimenti ya Wizara hiyo na kuyapitia maagizo yaliyotolewa katika kamati za Bunge kama yametekelezwa kabla ya kufanyika kwa vikao vya  kamati vya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania vinavyotarajiwa kuanza huku akiiagiza menejimenti ya wizara hii kuhakikisha mambo yanayohusiana na  sekta zote tatu kuzishirikisha  sekretarieti za mikoa ili yafahamike.

“Mambo ni mazuri yanayofanyika lakini je vipi kamati za ushuari za Wilaya na Mikoa zinayafahamu? Wabunge wanayafahamu kutoka majimboni mwao? Lazima mambo haya yafahamike kwa jamii. Shirikisheni maafisa michezo wa wilaya na mikoa, MakatibuTawala wa Wilaya  na Makatibu Tawala wa Mikoa yote. Mkifanya hivy yatapunguza maswali na malalamiko katika maendeleo ya sekta zetu za Utamaduni Sanaa na Michezo.”

Mheshimiwa Gekul amesema kuwa miongoni mwa maagizo ya mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kunakuwepo na shule za michezo zinazofundisha mchezo mmoja mmoja si jambo la busara kila shule ya michezo iwe na michezo yote.

“Kwa mfano mkoa wa Morogoro ni mzuri kwa ngumi tuwe na shule ya ngumi, Manyara ni mzuri wa riadhaa tuwe na shule ya riadha, sasa kama tunafundisha ubondia Manyara wakati hakutapatikana mabondia wazuri tutakosea.”

Kwa upande wake Mkurungenzi wa Maendeleo ya Michezo Nchini Ndugu Yusufu Singo amesema kuwa maelekezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri yamepokelewa na yanafanyiwa kazi.

Katika kikao hicho pia ilibainika kuwa michezo ya kubahatisha hadi sasa imeingiza serikali zaidi ya milioini 822.

Akizungumza mbele ya Naibu Waziri Gekul, Mkurugenzi wa Maandeleo ya Michezo kupitia BMT Ndugu Singo amesema  pesa hizo bado ni ndogo  ana  hakika zitaongezeka.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa nchini Dkt Emmanuel Ishengoma amesema  kuwa pasiposhaka ndani ya idara yake maaagizo kadhaa yamefanyiwa kazi.

“Kweli tumeyafanyia marekebisho mambo kadhaa ambayo kamati inayosimamia wizara yetu iliagiza na kimsingi viambatanisho vyote vimekamilika ili kamati ya Bunge kupelekewa mezani kwake.”

Kikao hiki kilikamilika baada ya kupitia maagizo yote yaliyotolewa na kamati.