Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa kwenye  runinga ya Fox News  amesema  mashambulizi ya Urusi  nchini Ukraine yaliyoanza Jumatano usiku wa kuamkia leo  yasingefanyika wala kutokea  wakati wa utawala wake.

Trump alipiga simu na kusema hakuamini kwamba Putin alitaka kufanya hivi mwanzoni.

"Nadhani alitaka kufanya jambo ili kufungua milango ya majadiliano, na hali ikawa mbaya zaidi, na ndipo akaona udhaifu," Trump alisema.

Zaidi ya hayo, Trump amesema kwamba anaamini uvamizi wa Urusi umechochewa kwa sehemu na "udhaifu" wa kujiondoa kwa Marekani  kutoka Afghanistan.