SERIKALI  kwa kushirikiana na kampuni  ya CRRC International  ya China wamesaini mkataba wa ununuzi  wa mabehewa 1,430 ya  mizigo ya Reli ya kisasa- SGR mkataba huo utakaogharimu  Dola za kimarekani  milioni 127.2.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa  Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa, amesema mkataba huu ni wa miezi kumi na mbili na utahusisha  usanifu na utengenezaji wa Mabehewa kwa ajili ya kubeba mizigo ya aina mbalimbali kulingana na aina ya behewa na matakwa ya mteja kupitia reli ya kisasa.

Aidha Kadogosa alisema ujio wa mabehewa hayo yatasaidia kusafirisha vitu mbalimbali kama Mifugo, Sukari, Chumvi, Pamba, Tumbaku, Kahawa na magari ambayo kwa kiasi kikubwa yanasaidia kukuza biashara ndani na nje ya nchi kama Uganda.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa  Shirika la Reli (TRC) Masanja Kadogosa amesema mkataba huu ni wa miezi kumi na mbili na utahusisha  usanifu na utengenezaji wa Mabehewa kwa ajili ya kubeba mizigo ya aina mbalimbali kulingana na aina ya behewa na matakwa ya mteja kupitia reli ya kisasa.

Aidha Kadogosa alisema ujio wa mabehewa haya yatasaidia kusafirisha vitu mbalimbali kama mifugo,sukari, chumvi, pamba, tumbako, Kahawa na magari ambazo kwa kiasi kikubwa zitasaidia kukuza biashara ndani na nje ya nchi kama Uganda, Rwanda, Burundi na congo kwa kurahisisha usafirishaji na kupunguza  gharama  za matengenezo ya barabara.

Pia Kadogosa alisema faida za mabehewa hayo ni kwamba yataraisisha biashara ya usafirishaji wa mizigo kupitia reli ya kisasa kwa umbali wa km 500, hivyo unatarajia kukamilika kwa manunuzi na kuwasili kwa mabehewa hayo February 2023.
 

Akizungumza katika Hafla hiyo leo jijini Dar es salaam Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame mbarawa Serikali imedhamiria kuhakikisha huduma ya usafiri wa mizigo inaimarika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kwa lengo la kuongeza pato la taifa na kukuza uchumi.

‘Ujenzi wa Reli ya kisasa unaoendelea hivi sasa kwa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro ambacho kimefika 95%, Morogoro – Makutupora ambacho kimefika 81% na kipande cha Mwanza – Isaka ambacho kimefika 4% ni ishara tosha kwamba Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuongeza ufanisi na kuboresha huduma ya usafiri na usafirishaji kupitia reli’amesema Waziri Prof Mbarawa.

Aidha,Profesa Mbarawa amesema kutokana na uwezo mkubwa wa reli ya kisasa Behewa hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza mrundikano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam ambapo treni moja itakuwa na uwezo wa kubeba Tani 10,000 kwa mkupuo ambayo ni sawa na malori 500.